Tanzania imeahirisha ombi la kuuza zaidi ya tani 100 za pembe za ndovu
ili kuendana na kanuni zilizowekwa na Mkataba wa Biashara ya Kimataifa
ya Wanyama na Viumbe Vilivyo Hatarini (CITES), liliripoti gazeti la
Tanzania la The Guardian hapo Jumatano (tarehe 2 Januari).
Tanzania itaongeza udhibiti dhid ya uwindaji haramu na kuimarisha
vikwazo vya magendo ya pembe za ndovu kabla ya kutuma tena ombi lake.
Serikali pia itafanya sensa ya idadi ya tembo kujua kiwango cha wanyama
hao nchini humo, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Utalii na Maliasili.
Tanzania imeomba kuuza pembe za ndovu zilizomo kwenye ghala yake,
zilizopatikana kutokana na tembo waliokufa vifo vya kawaida au
waliouliwa kwa sababu ya kuhatarisha maisha ya wanadamu, ili kugharamia
vyema programu zake za ulinzi wa rasilimali.
CITES ilikataa ombi kama hilo la serikali ya Tanzania mwaka 2010,
ikihoji kwamba kuzipeleka pembe hizo sokoni kungeliongeza, na sio
kupunguza, visa vya uwindaji haramu.
No comments:
Post a Comment