MAONI YA CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR(SUZA)YA KUPATA KABIBA MPYA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YATAKAYOWASILISHWA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA
ENEO: UKUMBI WA MIKUTANO MFUKO WA BARABARA ZANZIBAR
TAREHE 13 JANUARI,2013
ENEO LA MFUMO WA MUUNGANO NA UENDESHAJI WAKE
(1).Katiba itamke wazi kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inaundwa na Nchi mbili huru yaani Jamuhuri ya watu wa Zanzibar na Jamuhuri ya watu wa Tanganyika zenye haki sawa kwenye Muungano huo.
(2).Katiba mpya iweke wazi kwamba masuala yatayohusu Muungano wa chi mbili hizo,ikiwemo aina ya Muungano wenyewe baina ya nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar yaamuliwe na wananchi yaamuliwe na wananchiwe wenyewe wa nchi hizo kwa kupitia kura ya maoni sizizozidi miaka mitatu baada ya mchakato wa kutafuta katiba mpya utakapomalizika.
(3).Katiba itamke wazi utaratibu wa kuongeza Mambo ya muungano na uwe kwa makubaliano na ridhaa za pande zote mbili za jamuhuri ya watu wa Zanzibar na jamuhuri ya watu wa Tanganyika,lakini katika kupunguza au kuondosha jambo au mambo ya Muungano ridhaa au maaamuzi ya upande mmoja tu wa Muungano utosheleze kuliondosha jamo/mambo ya muungano (ridhaa kwa pande mbili katika kuondosha
mambo ya muungano isiwe lazima.
(4).Masuala yote ya Muungano,katiba iandike kwamba uwezo/mamlaka ya uanzishaji,uendeshaji na usimamizi wa mambo yote ya muungano katika kifungu cha 4 (3)Jadweli la kwanza,katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania 1997,yawe chini ya Raisi wa Zanzibar na yawe na hadhi ya kisheria kitaifa kikanda na kimataifa.
(6).Uteuzi wa nafasi za Taasisi za Muungano:uteuzi wa nafasi za Taasisi za muungano uwe a uwiano ulio sawa kwa pande zote mbili za Muungano (Jamuhuri ya watu wa Zanzibar na Jamuhuri ya watu wa Tanganyika)
(7).Aidha katiba itamke wazi vigenzo vya kitaaluma kwa wateuliwa wa nafasi katika taasisi za Muungano.
(8).Masuala/mambo ya nje:katiba itamke wazi kwamba Zanzibar itakuwa na Mamlaka kamili ya kisheria kwa mambo yote ya nje,katika hili Zanzibar kupitia Rais wake iwe na mamlaka /uwezo kamili wa kuingia mikataba,mashirikiano ya kimataifa,kujiunga na Taasisi au Jumuia mbali mbali za kimataifa na kimataifa kwa maslahi ya Jamuhuri ya watu wa Zanzibar.
(8).Suala la elimu ya Juu:mamlaka na uwezo ya uanzishaji ,usimamizi na muendeshaji wa masuala yote ya elimu ya juu Zanzibar yaw echini ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi akishirikiana na baraza la wawakilishi la Zanzibar na masuala hayo ya elimu ya juu kwa Zanzibar yawe na hadhi sawa ya kisheria kitaifa,kikanda na kimataifa.
(9).Suala la utafiti:uwezo wa uanzishaji,usimamizi na uendeshaji wa masuala yote ya tafiti na sayansi kwa upande wa Zanzibar yaw echini ya Raisi akishirikiana na Baraza la wawakilishi la Zanzibar na masuala hayo ua utafiti na Sayansi yawe na hadhi sawa ya kisheria ,kitaifa na uwakilishi nje ya Tanzania(kimataifa)
(10).Suala la baraza la mitihani la Taifa na nenmbo yote yanayohusika na kazi za Baraza;Uwezo a uanzishaji,usimamizi na uendeshaji wa masuala yote ya Baraza la Mitihani la Taifa kwa upande wa Zanzibar yawe chini ya Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi aishirikiana na baraza la wawakilishi la Zanzibar na masuala hayo ya baraza kwa Zanzibar yawe na hadhi sawa ya kisheria,kikanda na kimataifa kwa maslahi ya Jamuhuri ya watu wa Zanzibar.
(11).Mamlaka ya uanzishwaji wa vyuo vikuu vya Tanzania viliopo na vitakavyokuwepo Zanziar:Baraza la wawakilishi liwe na mamlaka kamli ya kuunda na kupitisha sheria zote za uanzishaji wa vyuo vikuu vitakavyokuweppo Zanzibar,na sheria hizo zitiwe saini na Rais wa Zanzibar.
(12).Pia katiba itamke wazi asilia ya mgawanyo wa nafasi za masomo ya Elimu ya juu zinazotolewa kama msaada (Scholarship za Muungano).
(13).Raisi wa Zanzibar awe na mamlaka kamili ya uwekaji sahihi wa chata za vyuo vikuuvyote vitakavyokuwepo Zanzibar na vyuo view na sifa na hadhi sawa ya kisheria nay a kitaifa na vile vyuo ambavyo sheria na chata zao zitasainiwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
(14).Waziri atakaehusika au kushughulikia Elimu Zanzibar awe ba nanlaka kamili ya Elimu ya Juu kwa upande wa Zanzibar na awe na mamlaka na hadhi sawa ya kisheria,kitaifa na uwakilishi sawa mwa Zanzibar nje ya Tanzania.
(15).Katiba itamke wazi juu ya mgao wa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu kwa vile ni ya Muuungano uwiano huo uwe sawa baina ya Wanafunzi wa Tanganyika na wa Zanzibar.
Kwa msaada wa Abdallah Abeid
No comments:
Post a Comment