
Jan
14
2013
Chama cha Mapinduzi (CCM)
kimesema kitaendelea kuimarisha mahusiano yake na taasisi mbalimbali za
kijamii na zile za kimataifa ili kuendeleza mashirikiano yaliyopo kwa
lengo la kukiimarisha chama hicho.
Akizungumza na vijana wa CCM
walio vyuo vikuu mbalimbali nchini Katibu wa Idara ya siasa, Itikadi na
Uhusiano wa Kimataifa Nd, Hamad Yussuf Masauni huko Afisi kuu ya CCM
Kisiwandui amesema, kuimarisha mashirikiano na taasisi hizo kutakijengea
msingi imara chama hicho katika kuongoza dola.
Nd, Masauni amesema kuwa Idara
ya siasa, Itikadi na Uenezi haina budi kufanya kazi kwa bidii ili
kukifanya chama hicho kupata ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.
Aidha Nd, Masauni amewataka
vijana hao kuendelea kutetea sera ya chama chao katika mfumo wa muundo
wa Muungano kuwa wa serikali mbili kwani ndio wenye maslahi kwa Zanzibar
na Tanzania kwa ujumla.
Pia amesema kuwa wanaotetea
mfumo wa Muungano wa mkataba na Serikali tatu wana lengo la kuvunja
Muungano jambo ambalo ni hatari kwa usalama wan chi na wananchi wake
hivyo hapana budi kupingwa kwa nguvu zote ili kuepusha athari zinazoweza
kutokea.
Akizungumzia faida za Muungano
Nd, Masauni amesema kuwa Muungano uliopo unfaida kubwa ikiwamo kukuwa
kwa uchumi wa nchi pamoja na kuimarika kwa mahusiano ya muda mrefu baina
ya Zanzibar na Tanzania Bara hivyo amewataka vijana hao kuendelea
kuutetea ili kuzidi kuimarisha Uchumi wa Nchi.
Pia amewataka vijana hao
kutumia kutumia taakuma waliyo nayo kuandaa makongamano na midahalo
mbalimbali ili kutoa taaluma kwa Wananchi juu ya faida zinazopatikana
ndani ya Muungano kwani wao ndio nguvu kazi ya Chama na tegemeo kwa
Taifa.
No comments:
Post a Comment