Mfuko wa Huduma za Dharura za Majanga (DREF) wa Shirikisho la
Kimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Mwekundu (IFRC) ulitangaza siku
za Jumanne (tarehe 15 Januari) kwamba imetenga kiasi cha dola 300,000
kuwasaidia watu 12,936 walioathiriwa na mafuriko katika majimbo ya
Nyanza na Bonde la Ufa nchini Kenya.
Mvua kubwa zilizoanza mwezi Disemba zimewaua watu 13 na kuwakosesha
makazi watu 765 huku wengine watano wakiwa bado hawajulikani walipo, kwa
mujibu wa IFRC. Watu waliobomolewa makaazi zao wanahifadhiwa kwa sasa
kwenye majengo ya shule, makanisa, maduka ya umma na miongoni mwa
familia wahisani, lakini wanafunzi watahitaji kuingia tena kurudi
mashuleni.
Fedha hizo za DREF utakiwezesha chama cha Msalaba Mwekundu cha Kenya
kuendelea na operesheni zake za kuwatafuta manusura na uokozi kwenye
eneo hilo, kuwafuatilia watu waliopotea na kutoa huduma muhimu za
chakula, maji safi na afya kwa watu walioathiriwa na mafuriko.
Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya inatabiri kwamba mvua zitaendelea
kipindi chote cha kati ya mwezi Januari, kwa mujibu wa Msalaba Mwekundu.
No comments:
Post a Comment