Thursday, January 17, 2013

Uhamaji kutoka Pembe ya Afrika kwenda Yemen yafikia kiwango cha juu

adi ya wahamiaji 107,500 walifanya safari ya kutoka Pembe ya Afrika kuelekea Yemen mwaka 2012, likiwa ni ongezeko la watu 103,000 waliofanya hivyo mwaka 2011, lilitangaza Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) hapo Jumanne (tarehe 15 Januari).
Zaidi za asilimia 80 ya wahamiaji hao walikuwa ni Waethiopia na waliobakia ni Wasomali. Wale wanaowasili kwenye fukwe za Yemen wanaitumia nchi hiyo kama njia ya kupita kuelekea nchi ya Ghuba.
Kuvuka huko ni hatari na shirika la UNHCR linakisia kwamba kiasi cha watu 100 walikufa maji wakiwa njiani. Wasafirishaji watu kwa magendo mara kadhaa huwalazimisha abiria kujirusha majini kuepuka walinzi wa pwani wa Yemen, na hivyo kusababisha wengi kufa maji, ilisema UNHCR.
Licha ya kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi na kiusalama, Yemen inawahifadhi zaidi za wakimbizi 236,000, karibia wote wakiwa Wasomali. Wasomali wanatambuliwa moja kwa moja kuwa wakimbizi wakiwasili tu Yemen.

No comments:

Post a Comment