Taarifa ya ofisi ya Mufti
Zanzibar imemtaka Bibi Salama Issa Kagire mwenyeji wa Tanzania Bara
ambae huja Zanzibar akidai kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu
kusitisha mara moja mihadharayake ya upotoshaji Waislam hapa nchini.
Taarifa hiyo iliyotolewa na
kusainiwa na Kaimu Katibu wa Mufti Zanzibar Sheikh Suleima Omar Jongo
imesemakuwa Bibi Salama amekuwa akija Zanzibar mara kwa mara akiendesha
mihadhara mbalimbali huku akijiita yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu jambo
ambalo mafundisho ya Uislamu yanapingana nalo,
Ofisi ya Mufti ilimwita Bibi
Kagire huko ofisi ya Mufti tarehe pili mwezi huu mbele ya Mufti na
Sheikh Saleh Omar Kabi pamoja na jopo la maulamaa wa Zanzibar ambapo
bila ya kisisi alithibitisha kauli yake hiyo ya kuudhalilisha Uislam
bila ya hoja ya msingi.
Awali katika kipindi cha nyuma
aliwahi kufika ofisini hapo kuomba kibali cha kufanya mihadhara ya
kawaida kwa Waislamu na kuruhusiwa na hatimae waislamu kulalamikia kauli
zake kuelekea kumkufuru Mwenyezi Mungu.
Alipoulizwa kuhusu hoja zake
amesema kuwa antumia Qur-ani hii iliyopo na kukiri kukosewa kwa baadhi
ya aya zilizomo ndani ya Qur-ni.
Kufuatia kadhia hiyo ofisi ya
Mufti Zanzibar imemtaka bibi huyo kutubia na kuacha mara moja kauli zake
hizo za kikafiri na endapo hatotubia uislamu utakuja unamsuta kwa aya
ya 40 ya SURATUL-AHZAAB inayoelezea kutokuja mtume mwengine ulimwenguni
baada yaa Mtume Muhammad (SAW).
Pia atakosa haki zote za
kisheria juu ya Uislam na kuingia msikitini na sehemu za Ibada kwake ni
kharam na wafuasi wake wametakiwa kutengana fikra hizo kwani umfuata mtu
huyu ni ukafiri.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizotokewa na mmoja wa wafuasi wa Bibi Kagire Nd, Ahmed Suleiman
Khamis mkaazi wa Darajabovu amekiri kuwepo wafuasi wa Bibi huyo
anaejiita Mtume na kwa Zanzibar wapo wafuasi wapatao mia mbili.
No comments:
Post a Comment