Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohammed Shein
ameuagiza uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzi ya Amali kuhakikisha
michezo yote inayoruhusiwa kisheria Zanzibar kuchezwa mashuleni
isipokuwa mchezo wa Ngumi (Boxing).
Amesema
michezo yote inafaa kuchezwa wala haipunguzi kasi ya mwanafunzi kusoma
na kwamba Wizara inapaswa kulisimamia agizo hilo ili Zanzibar iweze
kupata vipaji vitakavoiletea nchi Medali za mashindano ya kitaifa na
kimataifa.
Rais
Shein ameyasema hayo alipokuwa akizindua Mradi wa “Mpira Mmoja” “One
World Football ball Project for Africa” Wenye lengo la kupambana na
Ukatili dhidi ya Watoto kupitia mchezo wa Mpira katika Uwanja wa Aman
mjini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar.
Amesema
Mradi huo ambao umewalenga zaidi Wanafunzi wa Shule umefufua matumaini
mapya ya kuibua vipaji vya michezo mbalimbali Zanzibar na kwamba
kinachohitajika kwa sasa ni mipangilio mizuri kutoka kwa Walimu na
wasimamizi wa michezo mashuleni.
Aidha
amesisitiza kuwa michezo haimzuii mwanafunzi kufanya vizuri darasani
hivyo Wazazi na walezi waendelee kutoa mashirikiano kwa watoto wao
kuhusu michezo stahiki wanayoipenda.
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein akizindua Mradi Mkubwa wa Ugawaji wa
Mipira ya kuchezea kwa Vikundi mbalimbali vya Michezo hadi Mashuleni kwa
kuanza kumgawia kijana Yunus Fadhil Juma kutoka Mkoa wa Kusini Pemba
hafla iliofanyika hapo Uwanja wa Amani Zanzibar.
Rais
Shein alifahamisha kuwa mradi huo pia utasaidia sana kujenga kikosi
imara cha Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwa vile vipaji
vya Soka vitaibuka vingi mashuleni vitakavyosaidia Timu hiyo kuwa tishio
Afrika Mashariki na Kati.
Akigusia
suala la Zanzibar Heroes na ushindi wa nafasi ya tatu uliyoipata katika
Mashindano ya SECAFA Rais Shein amesema timu hiyo ilicheza vizuri kiasi
cha kumvutia sana na kuongeza kuwa Zawadi yao ipo kinachohitajika ni
kumalizwa tofauti baina ya Wachezaji na Viongozi wa Timu hiyo.

Waziri
wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akitoa hotuba ya
Kumkaribisha Rais wa Zanzibar ili kuwahutubia wananchi waliohudhuria
katika Uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Ugawaji Mipira ya kuchezea kwa
Vikundi mbalimbali vya Michezo hadi Mashuleni kwa Zanzibar nzima, hapo
Uwanja wa Amani Zanzibar.
Kwa
upande wake Waziri wa Habari na Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali
Mbarouk amesema Mradi huo umelenga kuleta vuguvugu la michezo na kuondoa
tatizo la vifaa vya michezo Zanzibar ili kuibua vipaji vitakavyoifanya
Zanzibar iwe tishio katika michezo mbalimbali.
Aidha
ameongeza kuwa Mipira hiyo itagaiwa katika maeneo yote ya Unguja na
Pemba bila ya upendeleo na kwamba Timu zote zilizosajiliwa na Makundi
maalum watanufaika na mipira hiyo.
Mradi
huo ambao umefadhiliwa na One World Futbal,Shirika la Kusaidia Watoto
Duniani kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar
unajumuisha Mipira-Elfu 20, itakayogaiwa kwa Wanafunzi wa shule na Timu
za Soka za Unguja na Pemba.
No comments:
Post a Comment