Rasi wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud hivi karibuni alikutana na
wanafunzi wa Somalia na wanachama wa jamii ya Wasomali katika mji mkuu
wa Sudani wa Khartoum, redio ya Bar-Kulan inayofadhiliwa na Umoja wa
Mataifa iliripoti Jumatano (tarehe 2 Januari).
Mohamud aliijulisha jamii hiyo kuhusu hali ya usalama nchini Somalia
na alisema serikali inawajibika kurejesha usalama. Pia aliishukuru
serikali ya Sudani kwa kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa
Somalia.
Mohamud aliwasili Sudan tarehe 1 Januari kusherehekea maadhimisho ya 57 ya uhuru wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment