Zanzibar imepanga kuzindua miradi 62 ya
maendeleo wakati wa wiki ya kuelekea siku ya uhuru tarehe 12 Januari,
kwa kuanza na zoezi la kufanya usafi nchi nzima (tarehe 4 Januari),
Daily News la Tanzania liliripoti.
Siku ya Jumamosi, Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein atafungua jengo
jipya la Taasisi ya Utawala wa Umma huko Tungu, na kituo kipya cha
udhibiti wa serikali huko Mazini, yote yalijengwa kwa fedha kutoka
serikali ya China.
Makamu wa Rais wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal atafungua hoteli ya
kitalii ya nyota tano katika kijiji cha Nungwi siku ya Jumapili, na siku
inayofuata ya Alhamisi Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete atafungua shule
mpya inayoitwa Mlimani.
Viongozi mashuhuri wa serikali wa Zanzibar na Tanzania wataendelea
kuongoza katika uzinduzi wa miradi kama hiyo kwa wiki nzima, ikiwa ni
pamoja na shule za sekondari, maabara za uchunguzi na mabweni ya
wanafunzi.
Waziri wa Nchi anayeshughulikia Matukio ya Kitaifa Mohamed Aboud
Mohamed alitetea sherehe hizo za muda mrefu, ambazo zinakadiriwa
kugharimu shilingi milioni 600 (dola 380,000). "Tusifikirie kwamba fedha
zinatumiwa kupita kiasi, zinatumiwa katika miradi ya maendeleo,"
alisema.
No comments:
Post a Comment