Raia wanane na wanamgambo 17 wa al-Shabaab waliripotiwa kuuawa kwenye operesheni hiyo, ambayo lilikuwa jaribio la idara ya ujasusi ya Ufaransa kumuokoa jasusi Denis Allex ambaye amekuwa akishilikiwa mateka na al-Shabaab tangu mwaka 2009.
Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa aliuawa wakati wa operesheni hiyo na mwengine aliripotiwa kukamatwa mateka na al-Shabaab. "Mwanajeshi huyo wa Ufaransa aliyekuwa kwenye uvamizi huo nchini Somalia alikufa kutokana na majeraha aliyopata," msemaji wa al-Shabaab Abdulaziz Abu Musab aliliambia shirika la habari la AFP. "Madaktari wetu walijaribu kumsaidia lakini hakuwa na bahati."
Wizara ya ulinzi ya Ufaransa hapo Jumatatu ilielezea wasiwasi wake kwamba al-Shabaab itaionesha miili ya mwanajeshi wake na Allex, ambaye Ufaransa wanaamini aliuawa wakati wa operesheni hiyo. Hata hivyo, al-Shabaab ilisema kwamba Allex yu hai na kwamba karibuni itatangaza hukumu yake juu ya majaliwa ya mateka huyo.
"Kila dalili kwa bahati mbaya zinatuongoza kuamini kwamba al-Shabaab inapanga kuonesha picha ya aibu na kuogofya" ya miili hiyo, alisema Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian
Tangu hapo al-Shabaab imetuma picha za mwili unaodhaniwa kuwa kamanda wa Kifaransa kwenye mtandao wake wa Twitter.
No comments:
Post a Comment