22 Februari, 2013 - Saa 10:10 GMT

Tembe za kuzuia mimba
Kanisa Katoliki
nchini Ujerumani limeamua kuwa ni halali kwa mwanamke kutumia tembe ya
kuzuia mimba mara tu baada ya kubakwa.
Uamuzi huu umefanywa kufuatia mkutano wa
viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Ujerumani baada ya mwanamke mmoja
aliyekuwa amebakwa kusema kuwa alizuiwa kufanyiwa matibabu siku mbili
mfululizo katika Hospitali zinazofadhiliwa na Kanisa Katoloki zikisema
kuwa kuzima mimba ni kinyume cha maongozi yake.Mwishowe Maaskofu hao walikubaliana kuwa itakuwa halali ikiwa tembe hizo zitatumiwa na mwanamke aliyebakwa kwa lengo la kuzuia kushika mimba badala ya kutoa mimba
Hii ina maana kuwa itaweza kutumiwa tu kama kifaa cha kuzuia kushika mimba lakini sio kuavya. Tembe hizo hutumiwa na wanawake wengi wasiotaka kushika mimba baada ya tendo la ndoa.
Hata hivyo Kanisa Katoliki nchini Ujerumani, ambako Papa wa sasa alitoka, limegawanyika kufuatia tendo hilo la ubakaji.
Ubishi kama huo nchini Marekani haukufikia uamuzi baada ya pande zote zilizokuwa zikibishania dawa hiyo kusema kuwa ni vigumu kujua kama baada ya kitendo cha ndoa asubuhi inayofuata mwanamke ameshika mimba au la.
No comments:
Post a Comment