Imewekwa na Mhammed Khamis
.Hii ndio hali halisi ya waendesha Gari za Ngombe wanavowatumia Wayama hawa kwa kujipatia Riziki zao
WIZARA
YA MIFUGO NA UVUVI IMEANDAA MPANGO MAALUM WA KUREKEBISHA SHERIA YA
WANYAMA ILI KUDHIBITI UDHALILISHAJI UNAOFANYWA KWA WANYAMA HAO.
AKIZUNGUMZA
NA MWANDISHI WETU MWANASHERIA WA WIZARA HIYO BI AMNE SAID AMESEMA
KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA UKATILI DHIDI YA WANYAMA SIKU HADI SIKU,
WIZARA HIYO IMEONA IPO HAJA YA KUBADILISHA BAADHI YA VIFUNGU VYA SHERIA
YA UKATILI DHIDI YA WANYAMA ILI KUPUNGUZA VITENDO HIVYO.
AMESEMA
MAREKEBISHO YA SHERIA HIYO IMEWEKA KIWANGO MAALUM CHA UBEBAJI WA MIZIGO
USIOZIDI KILO CHA UZITO WA MNYAMA HUYO NA KUTOBEBESHWA MIZIGO KWA
MNYAMA AMBAE HAJATIMIA UMRI WA MIAKA MIWILI.
AMESEMA
SHERIA HIYO IMEANDAA UTARATIBU KWA WANANCHI KUTOA MAONI YAO ILI KUFANYA
MAREKEBISHO YA SHERIA MPYA INAYOKWENDA NA WAKATI WA SASA.
AMEFAHAMSHA KUWA MTU YOYOTE ATAKAEMDHALILISHA MNYAMA ATALAZIMIKA KUMHUDUMIA HADI APONE PAMOJA KULIPA FAINI ILIYOWEKWA.
HIVYO
AMEWATAKA WAFUGAJI KUTOWAACHIA WANYAMA WAO OVYO NA KUWAWEKA KWENYE
MAZINGIRA MAZURI ILI KUMUONGEZEA KIPATO MFUGAJI NA KUEPUSHA UKATILI
DHIDI YA WANYAMA HAO.
No comments:
Post a Comment