Sunday, February 10, 2013

WAZANZIBAR ALFU HAMSINI HAWAJAOPEWA VITAMBULISHO YASEMA CUF

 
 
 
 
 
 
Rate This

 


Naibu katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Mh, Hamad Massoud Hamad akizungumza na wapenzi na wanachama wa CUF katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kaimu Naibu katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Mh, Hamad Massoud Hamad amesema ipo haja kwa Masheha nchini kubadilika na kwenda sambamba na mfumo wa serikali ya Umoja wa kitaifa iliyopo.
Akihutubia wapenzi na wanachama wa chama hicho katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja Mh, Hamad amesema bado utendaji wa masheha hao hauridhishi ikiwa ni pamoja na ukandamizaji dhidi ya wafuasi wa chama hicho.
Amesma kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya Masheha kuwanyima vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi wafuasi wa CUF walio na sifa za kupatiwa vitambulisho hivyo na badala yake kuwapa watoto ambao hawajatimiza umri pamoja na wageni.
Aidha amefahamisha kuwa lengo la kuwanyima vitambulisho wafuasi wa chama cha CUF ni kupunguza idadi ya wanachama wa chama hicho katika daftari la kudumu la wapiga kura katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini.
“Hawa wameishiwa wameona uwezo wa kuizuia CUF isishinde hawana kwa hiyo wanafanya hivi ili wawapunguze katika daftari la kudumu la wapiga kura lakini hawatofanikiwa ushindi utakuja tu” alisema Mh, Hamad.
Pia amesema kuwa zaidi ya Wazanzibari elfu hamsini walio na sifa za kupatiwa vitambulisho hivyo bado hawajapatiwa vitambulisho hivyo.
Nae mjumbe wa Baraza kuu la Uongozi la Taifa la Chama hicho ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mjimkongwe Mh, Ismail Jussa Ladhu amesema Wazanzibari hawana sababu ya kuendelea na mfumo wa Muungano uliopo kwani umekuwa ukiidumaza Zanzibar katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii.
Mh, Jussa amesemakuwa Zanzibar imekuwa ikishindwa kupiga hatua katika sekta ya uchumi kutokana na vianzio vyote vya mapato hasa vya kimataifa kuhodhiwa na serikali ya Muungano na kuifanya Zanzibar kuwa nyuma kimaendeleo siku hadi siku.
Amesema kuwa Zanzibar imekuwa ikishindwa kuingia mikataba mbalimbali ya kimataifa inayoweza kukuza uchumi wa Zanzibar kutokana na kutotambulika kama nchi.
Aidha amefahamisha kuwa kumekuwa na misaada mbalimbali inayotolewa na wahisani mbalimbali kwa ajili ya Tanzania na misaada hiyo imekuwa ikiishia mikononi mwa Tanganyika pekee bila ya Zanzibar kupata chochote.
Pia amesema kuwa chini ya mfumo wa Muungano uliopo hakuna mwananchi wa Zanzibar atakaepiga hatua kimaendeleo kutokana na nyanja zote za kiuchumi kumilikiwa na Tanganyika hivyo mfumo pekee utakao toa fursa kwa Wazanzibar kusonga mbele kimaendeleo ni mfumo wa Muungano wa Mkataba pekee.
“Mfumo wa Muungano wa Mkataba ndio utakaomuwezesha Mwananchi wa Zanzibar kupiga hatua kimaendeleo kwani utakuwa unatoa fursa kwa Wananchi wa pande zote mbili kuweza kupiga hatua kimaendeleo” alisema Mh, Jussa.
Akizungumza katika mkutano huo Mjumbe wa baraza kuu la uongozi la CUF taifa ambae pia ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mh, Nassor Ahmed mazrouy amewataka wanachama wa chama hicho kutowasikiliza viongozi wasioitakia mema Zanzibar kwa kutoa kauli za za uongo.
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa akiwahutubia Wananchi wa Nungwi katika Mkutano wa hadhara wa Chama cha wanancgi cuf
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa akiwahutubia Wananchi wa Nungwi katika Mkutano wa hadhara wa Chama cha wanancgi cuf
Amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya viongozi wamekuwa wakipita kwa wananchi na kusema serikali iliopo inaendeshwa kwa sera za vyama hivyo wananchi wote hawanabudi kufuata matakwa ya sera hizo.
Mh, Mazrouy amefahamisha kuwa serikali iliyopo haiendeshwi kwa sera za vyama bali inaendeshwa kwa kuzingatia mahitaji ya wananhi wa Zanzibar.
Mapema katika risala yao wanachama wa chama hicho wa Jimbo la Nungwi wamesema tatizo la utozwaji wa kodi mara mbili na bodi ya mapato Zanzibar (ZRB) pamoja na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kumekuwa kukiwarudisha nyuma katika juhudi za kujinasua na janga la Umasikini linalowakabili

No comments:

Post a Comment